IQNA

Dua ya Arafa na sherehe za Idul Adh'ha na Ghadir kufanyika katika kituo cha Imam Ali (as) mjini Vienna

10:45 - December 04, 2008
Habari ID: 1715743
Tarehe 8 na 9 Disemba kituo cha Kiislamu cha Imam Ali (as) mjini Vienna Austria kitawapokea waumini watakaokusanyika hapo kwa ajili ya kufanya amali za dua ya Arafa na Idul Adh'ha.
Amali na sherehe hizo zitaongozwa na mkuu wa kituo hicho, Hujjatul Islam wal Muslimeen Ramadhani. Akitangaza ratiba ya sherehe hizo katika mahojiano na mwandishi habari wa shirika la IQNA, Sayyid Amir Illahi, mmoja wa wasimamizi wa kituo hicho cha Kiislamu amesema kuwa, baada ya kuswaliwa swala ya Idul Adh'ha katika kituo hicho, hotuba za swala hiyo zitatolewa na Hujjatul Islam Ramadhani na kutangazwa moja kwa moja katika lugha nne za Kifarsi, Kijerumani, Kituruki na Kiarabu kwa watu watakaohudhuria sherehe hiyo. Ameendelea kusema kuwa, mbali na kuswaliwa swala hiyo, kituo hicho pia kitakuwa mwenyeji wa sherehe za Idul Ghadir zitakazofanyika tarehe 16 Disemba ambapo hutuba muhimu za sherehe hizo zitatolewa na Hujjatyul Islam wal Muslimeen Muizzi, Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Uingereza. Hutuba yake itahusu 'Ghadir, siku ya uimamu na uongozi.' Kasida na mashairi ya kuvutia pia yatasomwa katika sherehe hizo. 329121
captcha