Allamah Fadhlullah ambaye ni mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu mekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa ibada ya Hija akiitaja kuwa ni mkutano wa kulinda umoja na mshikamano wa Kiislamu na wenzo wa kukabiliana na njama zinazopangwa na maadui za kuwatenganisha Waislamu.
Mwanazuoni huyo mashuhuri wa Kiislamu ameitaja Hija kuwa ni msimu wa umoja na kuwakurubisha pamoja wafuasi wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu na kuondoa mivutano ya kimakundi.
Ofisi ya msomi huyo wa Kiislamu mjini Madina inapokea idadi kubwa ya mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kutoka nchi mbalimbali.
Ofisi hiyo inajihusisha na kuwaelimisha mahujaji namna ya kutekeleza ibada ya Hija na kutayarisha mihadhara kuhusu maudhui mbalimbali za Kiislamu. 329465