Duru ya pili ya mafunzo kwa maimamu wa swala ya jamaa katika Taasisi ya Wakatoliki wa Ufaransa ilianza Ijumaa tarehe 5 Disemba huko mjini Paris, ambapo wanafunzi kadhaa wa dini ya Kiislamu wanahudhuria.
Gazeti la Le Monde limeandika kuwa, kati ya wanafunzi 27 waliohudhuria duru ya kwanza ya masomo hayo kumi na tano walifanikiwa kupata vyeti vya kuhitimu masomo ya 'madhehebu na mawasiliano baina ya tamaduni.' Kutokana na kutoelewa lugha ya Kifaransa maimamu wengi wa swala iliyotajwa hawakufanikiwa kukamilisha vizuri duru ya kwanza ya masomo hayo. Duru hii ya pili imeandaliwa kwa ajili ya watu ambao hawakufanikiwa kupata vyeti katika duru ya kwanza.
Itakumbukwa hapa kwamba, maimamu wapatao 2000 wanajishughulisha na kuswalisha swala ya jamaa katika misikiti ya pembe mbalimbali za Ufaransa. Duru ya kwanza ya masomo hayo iliandaliwa kwa ushirikiano wa msikiti mkuu wa Ufaransa na Taasisi ya Wakatoliki wa nchi hiyo ili kuwafundisha maimamu masomo yanayohitajika katika uendeshaji wa shughuli zao. 330026