Hayo yamesemwa na Imamu wa swala ya Ijumaa ya msikiti wa Qatif huko Saudi Arabia Sheikh Hassan Saffar ambaye ameongeza kuwa kufuata mfumo wa Ahlubaiti wa Mtume kunadhihiri katika kutenda amali njema na kujiepusha na mambo yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu.
Sheikh Saffar amesisitiza kuwa Ahlubaiti wa Mtume daima walikuwa wakiusia kutenda amali njema na kujiepusha na haramu.
Mwanazuoni huyo wa madhehebu ya Shia wa Saudi Arabia ameashiria baraka za siku ya Arafa (tarehe 9 Dhilhija) na akasisitiza juu ya umuhimu wa kutekeleza amali mustahabu za siku hiyo ikiwa ni pamoja na kusoma dua ya Arafa, kufunga na kufanya ziara ya Imam Hussein (as). 330713