IQNA

Kuanza tamasha la Qur'ani Tukufu nchini Saudi Arabia

9:29 - December 08, 2008
Habari ID: 1717010
Tamasha la nne la kitaifa la Qur'ani Tukufu nchini Saudi Arabia lilianza Jumamosi ya atrehe 6 Disemba kwa udhamini wa Baraza Kuu la Utalii la Saudia huko katika mji wa Dammam.
Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Arabia la Riadh, sherehe za ufunguzi wa tamasha hilo zilihudhuriwa na Jalawi bin Abdul Aziz, Naibu wa Amir wa Jimbo la Mashariki la Saudi Arabia pamoja na wakuu wengine wa kieneo. Limehudhuriwa pia na wapenzi wa Qur'ani Tukufu. Maonyesho ya Qur'ani, mashindano ya Qur'ani na ya kiutamaduni, michezo ya kuigiza inayohusianana visa vya Qur'ani na vilevile vikao mbalimbali vinavyohusiana na Qur'ani ni baadhi ya ratiba za tamasha hilo. Mbali na kuonyeshwa Qur'ani kubwa na ndogo zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu, na vilevile Qur'ani nyinginezo kongwe zilizoandikwa kwa mkono katika zama mbalibali za historia ya Kiislamu, bidhaa za sanaa ya mikono pia zitaonyeshwa katika maonyesho yatakayoandaliwa kwenye tamasha hilo. Tamasha hilo litaendelea kwa mufda wa wiki moja na baada ya kumalizika sherehe za siku kuu ya Idul Adh-ha, litawakaribisha mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu kulitembelea. Ratiba maalumu pia zitatekelezwa katika tamasha hilo kwa mnasaba huo adhimu. 330970
captcha