IQNA

Hatua kali za usalama nchini Iraq kwa mnasaba wa Idul Adh’ha

10:22 - December 09, 2008
Habari ID: 1717407
Viongozi wa Iraq wametangaza habari ya kuwekwa askari usalama wapatao elfu 34 katika miji ya Baghdad na Najaf kwa mnasaba wa kuwadia Idul Adh’ha.
Kuhusiana na suala hilo, serikali ya Iraq imewataka wananchi wasiegeze magari yao katika barabara kuu za miji hiyo na karibu na maeneo ya kidini na masoko ili kuzuia uwezekano wa kutokea milipuko ya kigaidi katika maeneo hayo. Wakati huohuo, askari usalama wa Iraq wametoa taarifa wakiwataka Wairaqi wote kushirikiana nao katika kudhamini usalama na kuzuia kutokea kwa vitendo vya ugaidi katika siku hii muhimu. Taarifa hiyo imewataka polisi pia kuchukua hatua za ziada za usalama na kutumia kila mbinu ili kuzuia vitendo vya utumiaji nguvu na ugaidi katika maeneo nyeti ya nchi hiyo. 331476
captcha