IQNA

Kituo cha upashaji habari cha "Uislamu" chafunguliwa Ujerumani

12:53 - December 10, 2008
Habari ID: 1717688
Kituo cha Upashaji habari cha Uislamu kimefunguliwa katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin katika sherehe zilizohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Wolfgang Schauble.
Shughuli za kituo hicho cha upashaji habari cha Kiislamu zitasimamiwa na serikali ya Ujerumani.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani amesema katika uzinduzi wa kituo hicho cha intaneti kuwa kazi hiyo ni hatua ya kuimarisha mazungumzo kati ya Uislamu na Ukristo na ameitaja kuwa ni zawadi kwa Waislamu kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul Haji.
Wolfgang ameashiria kwamba maudhui ya kituo hicho kwa mwezi huu ni "Uislamu Katika Maisha ya Kila Siku" na kuongeza kuwa, jumuiya na taasisi za Kiislamu zinaweza kutuma maudhui zao kwa kituo hicho kwa ajili ya uchambuzi na uchunguzi. 332027

captcha