Sheikh Ali al-Hashimi, mshauri wa masuala ya kidini katika serikali ya Imarati amesisitiza katika hotuba ya Idul Adh’ha juu ya umuhimu wa kuwepo umoja miongoni mwa Waislamu ili kutukuzwa na kuimarishwa Uislamu duniani.
Amesema, Waislamu wanahitaji kuwa na umoja ili kuenezwa thamani za Kiislamu ulimwenguni ukiwemo usamehevu, urafiki na maadili ya kiutu na kibinadamu. Ameashiria umuhimu wa Idul Adh’ha na kusisitiza kwamba, katika siku hii Waislamu wanapasa kuimarisha mazungumzo na kutembeleana ili kuimarisha umoja na udugu kati yao.
Swala ya Idi ya nchi hiyo iliongozwa na Sheikh Khalid bin Zayid Al Nahyan katika msikiti wa Sheikh Zayid bin Sultan Al Nahyan katika mji wa Abu Dhabi. Shakhsia kadhaa wa kidini, watawala, wanadiplomasia, mawaziri na viongozi wa kijeshi pia walishiriki katika sherehe hizo za Idul Adh’ha. 331650