Akizungumza eti kwa mnasaba wa Idul-Adh'ha katika mji wa Sakhnin amewataka viongozi wa Kiislamu kuwa na mitazamo aliyoitaja kuwa ya wastani, udugu na kuleta amani baina ya mataifa na wafuasi wa dini mbalimbali.
Matamshi hayo ya dhihaki ya Peres yanatolewa wakati ambao utawala ghasibu wa Israel unaendeleza jinai na ukatili dhidi ya Wapalestina hasa wakazi wa Ukanda wa Ghaza.
Nukta nyingine ya kuzingatiwa ni kuwa hivi karibuni viongozi watenda jinai wa utawala haramu wa Israel katika hatua ya kutaka kupenya katika ulimwengu wa Kiislamu walishiriki katika kongamano la Mazungumzo Baina ya Dini huko New York. Katika kongamano hilo, Mzayuni Peres ambaye ni gaidi na mtenda jinai za kivita alikuwa na mkutano wa kusikitisha na Sayyid Muhammad Tantawi, Sheikh wa Al Azhar na kutumia fursa huyo kuendeleza jitihada zisizo na natija wala faida za Israel za kujaribu kuanzisha uhusiano wa kawaida na nchi za Kiislamu. 332213