IQNA

Wasanifu majengo wa Uingereza kukarabati Masjidul Haram

11:39 - December 13, 2008
Habari ID: 1718438
Wasanifu majengo mashuhuri wa Uingereza wamealikwa na Mfalme Abdullah bin Abdulaziz wa Saudi Arabia kwa ajili ya kukarabati na kupanua msikiti mtukufu wa Makka.
Norman Foster na Zaha Hadid ni miongoni mwa wasanifu majengo maarufu wa Uingereza walioalikwa na Mfalme wa Saudia kwa ajili ya kazi ya kupanua na kukarabati Masjidul Haram, jengo la kihistoria na takatifu kwa Waislamu wote duniani.
Kwa sasa msikiti huo ambao kila mwaka hupokea zaidi ya mahujaji milioni tatu wanaokwenda kutekeleza ibada ya hija, unaweza kutumiwa na watu laki tisa na baada ya kufanyiwa marekebisho utakuwa na uwezo wa kupokea mara tatu zaidi ya idadi hiyo kwa mujibu wa matamshi ya viongozi wa Saudia.
Ukarabati huo utafanyika katika awamu mbili. Katika awamu ya kwanza utapanuliwa na kuwa na uwezo wa kupokea mahujaji milioni moja na nusu na baadaye utapanuliwa zaidi na kutumiwa na mahujaji milioni tatu kwa wakati mmoja. 332659

captcha