IQNA

Kuanza kikao cha kwanza cha Kiislamu cha haki za binadamu nchini Qatar

18:34 - December 15, 2008
Habari ID: 1719538
Kikao cha kwanza cha Kiislamu cha haki za binadamu kimefanyika huko mjini Doha Qatar, kwa mnasaba wa kuwadia mwaka wa 60 wa kutangazwa Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu. Kikao hicho cha siku mbili kimefanyika kwa udhamini wa Kamati ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Qatar na kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.
Mawaziri wa sheria wa nchi za Kiislamu, Katibu Mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Qatar, katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na kieneo yanayohusiana na masuala ya haki za binadamu ni baadhi ya watu walioshiriki katika kikao hicho. Katibu mkuu wa kamati hiyo ya Qatar amesema kuwa kikao hicho kimefanyika kwa shabaha ya kuimarisha haki za binadamu katika nchi za Kiislamu. Amesema kamati hiyo itafuatilia kwa karibu kupitishwa kwa hati ya haki za Kiislamu, hati ambayo imekuwa ikisisitizwa pia na Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC. Kati hiyo pia imeandaa warshi za mafunzo ili kufuatilia kwa karibu jambo hilo. 333669
captcha