Katika sherehe hizo ambazo zitahudhuriwa na shakhsia kadhaa na wataalamu wa Qur’ani Tukufu kutaonyeshwa msahafu wa Nur ulioandikwa katika karne ya 10 Hijria. Msahafu huo ambao hati zake ziliandikwa na msanii Nuruddin Muhammad katika mwaka 900 hadi 950 Hijria umenakshiwa kwa maji ya dhahabu na wasanii wa Iran. Urembo uliotumika kuinakishi nakala hiyo na msahafu ni maarufu katika maeneo ya Khurasan na Harat.
Nakala hiyo ya msahafu ulionakshiwa na kupambwa kwa maji ya dhahabu ni kazi ya miongo tisa ya wasanii na wataalamu wa kaligrafia wa Iran.
Maonyesho ya msahafu huo yatafanyika katika jumba la makumbusho la taifa la Qur’ani Tukufu mjini Tehran. 334217