IQNA

Mwenyekiti wa Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Ufaransa:

Serikali ibuni sheria za kupambana na propaganda chafu dhidi ya Uislamu

10:55 - December 23, 2008
Habari ID: 1721862
Mwenyekiti wa Muungano wa Jumuiya za Kiislamu nchini Ufaransa ameitaka serikali ya nchi hiyo kubuni sheria za kupambana na propaganda chafu dhidi ya Uislamu.
Ombi hilo limetolewa baada ya kuchomwa moto msikiti mmoja wa eneo la Saint-Priest katika viunga vya mji wa Lyon.
Tahami Bariz amesema: Serikali ya Ufaransa haipaswi kutosheka na kulaani kwa maneno vitendo vinavyovunjia heshima Uislamu na Waislamu, bali ibuni sheria za kupambana na propaganda chafu dhidi ya dini hiyo.
Tahami Bariz amesema kuwa Uislamu ni dini yenye nafasi kubwa katika jamii ya Ufaransa na inakubalika kati ya wananchi na katika serikali.
Mwenyekiti wa Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Ufaransa amempongeza Rais Nicolas Sarkozy wa nchi hiyo kwa kulaani kitendo cha kuchomwa moto msikiti wa Saint-Priest na akasema: Waislamu wa Ufaransa wanaheshimu katiba ya nchi hiyo na wanazingtia sheria za kijamii za taifa wakati wa kutekeleza ibada na ada zao za kidini. 337088
captcha