IQNA

OIC kuimarisha zaidi uhusiano wake na Russia

17:24 - December 24, 2008
Habari ID: 1722560
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) Ekmeleddin Ihsanoglu amesema kuwa suala la kuimarisha uhusiano kati ya ulimwengu wa Kiislamu la Russia katika nyanja mbalimbali linapewa umuhimu wa Kistratijia na jumuiya hiyo.
Ihsanoglu ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia mjini Jiddah, Saudi Arabia. Amesema kuwa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu iko tayari kushirikiana na Russia katika nyanja mbalimbali.
Ihsanoglu ameashiria uhusiano mzuri wa Moscow na nchi za Kiislamu na akasema: Uamuzi wa Russia wa kuainisha mwakilishi wa kudumu katika OIC ni hatua muhimu katika njia ya kuimarisha uhusiano wa nchi hiyo na ulimwengu wa Kiislamu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Sergei Varshinin amemkabidhi Katibu Mkuu wa OIC barua kutoka kwa Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia. Katika barua hiyo Lavrov amesisitiza juu ya kuimarishwa uhusiano wa Russia na nchi za Kiislamu katika nyanja mbalimbali za kiutamaduni, kijamii, kisiasa, kiuchumi na kibiashara. 337231

captcha