Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Arabia la al-Watan, Nick Pisgaman, mwanachama wa Kamati Kuu ya Idara ya kituo hicho cha utafiti amesema kuwa kituo hicho kimekuwa kikipata misaada kutoka kwa wizara hiyo na vilevile vyuo vikuu kadhaa vya Ulaya.Amesema, baada ya kukatwa misaada hiyo kituo hicho cha utafiti wa Kiislamu hakina tena uwezo wa kudhamini kifedha shughuli zake na kwa hivyo kitalazimika kufunga shughuli hizo kuanzia tarehe Mosi Januari. Pisgaman amesisistiza kwamba, kituo hicho kimekuwa na mchango muhimu katika kuondoa mivutano na hitilafu kati ya Waislamu na Wakristo na kuwafanya waishi pamoja kwa amani nchini Uholanzi. Ameendelea kusema kuwa, kufungwa kituo hicho cha Kiislamu nchini humo kutokana na sababu za kifedha ni mkasa mkubwa na kuongeza kwamba, Waislamu waliowachache na Wakristo wa msimamo wa wastani wana wasiwasi mkubwa kuhusiana na kufungwa kituo hicho.
Kituo cha Utafiti wa Kiislamu cha Uholanzi ambacho kiko katika mji wa Leiden ni kituo kikongwe zaidi ambacho kilianzishwa mwaka 1998 kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya sayansi, elimu, utamaduni na utafiti wa Kiislamu. 338401