IQNA

Wazayuni wataka kuzima sauti za wapigania uhuru katika Mashariki ya Kati

12:57 - December 28, 2008
Habari ID: 1723711
Kufuatia mapambano ambayo yamekuwa yakionyeshwa na wananchi wa Palestina hasa uungaji mkono wao mkubwa kwa serikali waliyoichagua wenyewe na inayoongozwa na Ismail Haniyya, Wazayuni wa Israel wana azma ya kuzima sauti za wapigania uhuru katika eneo nyeti la Mashariki ya Kati.
Akizungumzia suala hilo katika mazungumzo maalumu na mwandishi wa IQNA, Hujjatul Islam wal Muslimeen Sayyid Muhammad Jaafar Sadaat Musawi, mtaalamu wa masuala ya kisiasa ameashiria jinai za hivi karibuni za utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kusema kuwa, jinai hizo zinaashiria wazi kwamba utawala huo umeazimia kuzidhibiti ardhi zaidi za Waarabu pamoja na serikali zao. Amesema, pamoja na jinai zote ambazo zimekuwa zikitekelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Palestina, lakini msimamo wao thabiti dhidi ya jinai na unyama wa utawala huo umeupelekea utawala huo kutofikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina na hasa katika Ukanda wa Gaza. Amesema misimamo dhaifu ambayo imekuwa ikionyeshwa na baadhi ya nchi za Kiarabu na hasa ya watawala wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika kukabiliana na siasa za ukandamizaji za Wazayuni, imepelekea wananchi wa Palestina kupuuza misimamo hiyo na kuchagua njia ya mapambano kama njia pekee ya kukabiliana na jinai za utawala wa Israel dhidi yao. Amesema, jambo la kusikitisha ni kuwa badala ya nchi hizo kukabiliana na jinai za utawala haramu wa Israel, zimekuwa zikishiriakiana na utawala huo katika kuwakandamiza ndugu zao wasiokubaliana na siasa zao dhaifu mbele ya jinai za Wazayuni.332984
captcha