IQNA

Askofu Mkuu wa Canada:

Mashambulio ya anga ya Israel huko Gaza ni jinai dhidi ya binadamu

10:35 - December 29, 2008
Habari ID: 1724170
Mashambulio ya anga ya Israel huko Gaza ni jinai dhidi ya binadamu Askofu Mkuu wa Canada amelaani vikali mashambulizi ya ndege za kivita za Israel dhidi ya eneo la Ukanda wa Gaza na kuyataja kuwa ni jinai dhidi ya binadamu.
Askofu Roger Abasha ambaye anaongoza ujumbe wa Kanisa la Orthodox la Canada katika mji wa Quds huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, amesema kuwa mauaji ya umati yanayofanywa dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza katika kipindi hiki cha kukaribia mwaka mpya wa Miladia ni kitendo cha kuumiza na kusikitisha.
Askofu Mkuu wa Canada amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusimamisha haraka iwezekanavyo ukatili na vitendo visivyokuwa vya kibinadamu vinavyofanywa na Israel dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza. 339574

captcha