IQNA

Kikao cha dharura cha Umoja wa Nchi za Kiislamu kufanyika Jiddah

11:01 - January 01, 2009
Habari ID: 1725889
Kikao cha dharura cha Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC kimepangwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 3 Januari huko Jiddah nchini Saudi Arabia kwa lengo la kuchunguza na kujadili hali ya mgogoro wa Ukanda wa Gaza. Ripoti zinasema kwamba, kikao hicho kitafanyika kwa kiwango cha kamati andamizi ya jumuiya hiyo.
Akiashiria kwamba Iran na Uturuki zitahudhuria kikao hicho, mmoja wa viongozi wa umoja huo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa nchi nyingine muhimu za jumuiya hiyo zikiwemo za Syria, Pakistan, Senegal, Saudi Arabia na Palestina pia zimealikwa kushiriki. Wakati huohuo, Rais Abdallah Wade wa Senegal ambaye nchi yake ndiyo inayoshikilia kwa hivi sasa uwenyekiti wa OIC, amesema kwamba Khalid Mash'al, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas amesema kuwa Hamas iko tayari kusimamisha vita iwapo utawala haramu wa Israel utatangaza kusitisha vita na kuuondolea mzingiro wake wa kidhulma dhidi ya Ukanda wa Gaza. 341405
captcha