IQNA

Kuanza kikao cha kimataifa cha ‘mazungumzo ya Uislamu na Magharibi’ mjini Cairo

11:48 - January 04, 2009
Habari ID: 1726890
Kikao cha kimataifa cha ‘mazungumzo ya Uislamu na Magharibi’ kimeanza huko Cairo, mji mkuu wa Misri, kwa udhamini wa Chuo Kikuu cha al-Azhar.
Gazeti la nchi hiyo la al-Akhbar limesema kuwa katika kikao hicho, wanazuoni na wasomi wa Kiislamu na Kikristo kutoka nchi mbalimbali za dunia pamoja na mabalozi wa nchi za Kiarabu na za kigeni wanaohudumu nchini Misri watajadili na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala ya kidini na tamaduni mbalimbali. Ahmad at-Tayyib, mmoja wa wakuu wa Chuo cha al-Azhar amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, kikao hicho cha siku tatu pia kitajadili mivutano na masuala yanayozusha hitilafu kati ya pande mbili za Kiislamu na Magharibi na kuimarisha fikra za kuwafanya wafuasia na waungaji mkono wa thamani za Mashariki na Magharibi kuishi pamoja kwa amani. Ameongeza kuwa, washiriki wa kikao hicho watafanya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa Chuo Kikuu cha al-Azhar na taasisi nyingine za Magharibi zinazojihusisha na masuala ya kuimarisha mazungumzo kati ya dini mbalimbali. Abdu Daim Nassir, Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha al-Azhar amesema kuwa, kikao hicho pia kitachunguza njia za kuamiliana Waislamu na wafuasi wa dini nyinginezo, kupambana na vitendo vya utumiaji nguvu, mitazamo ya kupindukia mipaka, kuimarisha amani na mshikamano kati ya Waislamu na wafuasi wa dini nyinginezo. 342844
captcha