IQNA

Kushadidi maafa ya kibinadamu Gaza, kivuko cha Rafah kingali kimefungwa

15:05 - January 06, 2009
Habari ID: 1728089
Wakuu wa Misri wameendelea kufunga kituo cha mpakani cha Rafah ambacho ndio njia pekee ya kuingiza misaada ya kibinadamu na kuwaondoa majeruhi katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Syria (SANA), Salem Chaa’chaa, Msemaji wa Shirika la Kuwasaidia na Kuwashughulikia Wakimbizi wa Palestina, kumejitokeza maafa ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kutokana na kuendelea hujuma ya utawala wa Kizayuni na hatua ya Misri ya kuendelea kufunga kituo cha mpakani cha Rafah ambacho ndio njia pekee ya kuwafikishia misaada ya kibinadamu wakazi wa eneo hilo.
Ameongeza kuwa, wanajeshi katili wa utawala haramu wa Israel wanazishambulia gari za kubebea wagonjwa na kuongeza kuwa imekuwa vigumu kuwasafirisha mashahidi na majeruhi.
Wakati huo huo televisheni ya Al Jazeera imeripoti kuwa kufungwa kituo cha Rafah kumepelekea trela kadhaa kutoka nchi za Kiarabu na Kiislamu zinazosheheni misaada ya kibinadamu kusubiri kwa siku kadhaa huku wakuu wa Misri wakikataa kutoa idhini ya kuingia Gaza au kusafirisha majeruhi kutoka eneo hilo. 344385
captcha