Taarifa hiyo imesema kuwa pamoja na kuwepo kwa zaidi ya vyuo vikuu 450 nchini Marekani lakini hakuna wahadhiri wala wanachuo wowote wa vyuo vikuu hivyo ambao wamejitokeza na kulaani kitendo hicho cha kinyama cha Wazayuni dhidi ya chuo kikuu hicho cha Gaza. Wakisisitiza kuwa chuo kikuu hicho kilikuwa moja ya vyuo vikuu muhimu zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati, wahadhiri hao wa Kiyahudi wamesema kuwa askari vamizi wa Kizayuni wamewanyima Wapalestina haki ya kupata elimu kwa kumoboa mashule, kukalia kwa mabavu ardhi, kushambulia kinyama, kufyatua risasi na kuwakagua kibaguzi na bila ya sababu yoyote muhimu wanafunzi na wanachuo wa Kipalestina.
Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza kilicholipuliwa na kubomolewa hivi karibuni na utawala haramu wa Israel kilikuwa na vyuo vingine 10 tanzu na wanachuo 20,000. 344217