IQNA

Makundi ya Malaysia yataka kususiwa bidhaa za Marekani

15:25 - January 10, 2009
Habari ID: 1729002
Kufuatia kuendelea jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza, makundi ya Kiislamu ya Malaysia jana Ijumaa yalitoa wito wa kususiwa bidhaa zote za Marekani nchini humo.
Makundi hayo yamesema kuwa wito wao huo unatokana na hatua ya serikali ya Washington ya kuunga mkono na kushirikiana na utawala huo katika kuendesha mauaji ya umati na jinai dhidi ya watu wasio na hatia wala ulinzi katika Ukanda wa Gaza.
Wito huo umetolewa katika hali ambayo hiyo jana maelfu ya waandamanaji wa nchi hiyo walifanya maandamano makubwa na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Kuala Lumpur kwa lengo la kulalamikia siasa za nchi hiyo katika kuunga mkono jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya wakazi wa Palestina. Pia waliitaka serikali ya Malaysia kufutilia mbali mikataba yote ya kiuchumi na kibiasha kati ya nchi hiyo na Marekani.
Akizungumza katika maandamano hayo, Mahathir Muhammad, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia amewataka wananchi wa nchi hiyo kutotumia sarafu ya dola ya Marekani kama alama ya malalamiko yao dhidi ya siasa hizo za Marekani na kusisitiza kwamba, iwapo watafanya hivyo, basi thamani ya sarafu hiyo itashuka.
Akizungumza katika maandamano hayo pia, Ma’mur Othman, mmoja wa wanachama wa Jumuiya ya Watumiaji Bidhaa ya Malasia amesema kuwa iwapo Waislamu wote watasusia bidhaa za Marekani hilo litakuwa ni somo zuri kwa utawala haramu wa Israel na washiraka wake ulimwenguni. 345723
captcha