Kwa mujibu wa Talal Dhafiri, mkuu wa jumuiya hiyo, mpango huo ambao utatekelezwa kupitia darsa za mafunzo ya Qur’ani katika vituo vya kuhifadhi Qur’ani katika pembe zote za Kuwait, una lengo la kusambaza utamaduni wa kitabu hicho kitakatibu katika jamii ya Kuwait. Amesema katika mpango huo wa Nifunze Qur’ani, ambao utaendelea kwa muda wa mwezi mmoja, mbali na wanachuo wa vituo vya mafunzo ya Qur’ani, matabaka mbalimbali ya wananchi wa Kuwait pia yanaweza kushiriki katika mafunzo hayo.
Dhafiri amesema mwishoni mwa mazungumzo yake na waandishi habari kwamba, mpango huo utajumuisha kuhifadhi, kusoma, tajweed, tafsiri na usomaji wa pamoja wa Qur’ani Tukufu. Visa vya Qur’ani pia vimezingatiwa katika mpango huo. 345504