Jmuiya ya Kimataifa ya Washairi ambayo ina zaidi ya wanachama 5000 kote ulimwenguni, imetoa taarifa huko Chile, makao makuu yake, ikilaani kuendelea kwa mauaji ya umati dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza.
Luis Aryas Manto, mkuu wa jumuiya hiyo amesema kuwa mashambulio ya kinyama yanayofanywa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza ni njama ya Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya kwa ajili ya kukandamiza mapambano ya wananchi wa Palestina. Amesema, kunyamaza kimya mbele ya jinai hizo ni sawa na kushirikiana na Wazayuni katika utekelezaji wa jinai hizo na kuwataka waandishi, washairi na wasomi mbalimbali wa ulimwengu kutumia ujuzi wao katika kulaani na kufanya juhudi za kusimamisha mashambulio hayo.
Amesema, jumuiya hiyo haitakaa kimya kuhusiana na jinai na mauaji yanayofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya wakazi wasio na hatia wa Ukanda wa Gaza na hasa watoto na wanawake na kusema kuwa washairi, wanachama wa jumuiya hiyo, watasoma mashairi yanayoulaani utawala huo kutokana na jinai zake hizo dhidi ya watu wasio na ulinzi.
Katika upande wa pili, Najib Khadari, Mkuu wa Jumuiya ya Washairi wa Morocco pia ametoa taarifa akisema kuwa utawala wa Israel ndio chanzo kikuu cha kuenea vitendo vya mabavu na misimamo ya kupindukia mipaka ulimwenguni na kuutaja utawala huo kuwa donda la kensa katika ulimwengu wa Kiarabu. 346490