IQNA

Kuanza kongamano la tisa la taasisi za kifedha Kuwait

14:04 - January 12, 2009
Habari ID: 1729665
Kikao cha tisa cha taasisi za kifedha za Kiislamu kilianza Jumapili nchini Kuwait kwa hisani ya shirika la Ernst & Young.
Kwa mujibu wa gazeti la Kuwait la Al Qabas, kongamano hilo la siku mbili linafanyika chini ya anwani ya “Sekta ya Kiislamu ya Fedha: Mtazamo wa Kisheria”.
Washiriki katika kikao hicho cha Kuwait ni wataalamu wa kifedha na wawekezaji kutoka nchi mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu.
Ajenda kuu ya mkutano huo ni kujadili utoaji huduma za kifedha kwa msingi wa sheria za Kiislamu, kuimarisha huduma za elektroniki katika taasisi za kifedha za Kiislamu, kustawisha uwekezaji wa Kiislamu Mashariki ya Kati na kukabiliana na mgogoro wa kifedha duniani.
Shirika la Ernst & Young limeanzisha taasisi za kifedha za Kiislamu katika nchi za Bahrain na Kuwati na taasisi hizo zinaendesha shughuli za kifedha na kibenki kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
Benki na taasisi hizo za kifedha za Kiislamu zilizoanzishwa kupitia shirika hilo zina majopo ya watafiti na wataalamu wa mausla ya uchumi wa Kiislamu. 346233
captcha