IQNA

UNESCO yalaani kuvamiwa vyombo vya habari Gaza

11:32 - January 14, 2009
Habari ID: 1730703
Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Koïchiro Matsuura amelaani hatua ya wanajeshi wa Israel kulenga ofisi za televisheni za satalaiti za Al Alam na Press TV.
Katika taarifa iliyotolewa katika makao makuu ya UNESCO mjini Paris, Matsuura amesema kuwa: “Kwa kushambulia ofisi za kanali za Iran za Al Alam na Press TV na kumuua Basel Faraj mwandishi habari wa televishein ya Algeria, Israel imekiuka azimio nambari 1738 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kinga ya waandishi habari katika oparesheni za kijeshi”.
“Israel inapaswa kuheshimu haki za waandishi habari katika utekelezaji kazi zao za kuakishi habari za matukio ya kieneo na kuacha kuficha habari za jinai za Gaza”.
Basel Faraj mwandishi habari wa televisheni ya ENTV ya Algeria aliaga dunia tarehe 6 Januari kufuatia majeraha aliyopata katika hujuma ya anga ya ndege za kivita za Israel huko Ghaza tarehe 27 December.
Aidha katika hujuma inayoendelea ya Israel katika Ukanda wa Gaza, hadi sasa waandishi wengine watatu wa habari wameshauawa.
Tarehe 9 Januari ofisi za kanali za televisheni za Iran za Al Alam ya lugha ya Kiarabu na Press TV ya lugha ya Kiingereza huko Gaza zilishambuliwa na vikosi vya utawala haramu wa Israel. 347631
captcha