IQNA

Jumba la makumbusho la 'Holocaust ya Gaza' lazinduliwa Misri

14:03 - January 14, 2009
Habari ID: 1731021
Jumba la makumbusho la elektroniki la "Holocaust ya Gaza" limezinduliwa katika kituo cha upashaji habari cha Secondlife.com. Jumba hilo la elektroniki limefunguliwa kwa hima ya Jumuiya ya Waandishi habari wa Misri.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi Habari ya Misri Abir Sa'di amesema kuwa katika jumba jilo la makumbusho la elektroniki kuna picha za vitendo vya kinyama na mauaji yanayofanywa hivi sasa na jeshi la Israel dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza.
Bibi Sa'di amesema kuwa mapambano dhidi ya jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza yanajumuisha medani ya elektroniki na kuongeza kuwa, lengo la maonyesho hayo ni kuweka wazi zaidi maafa ya jinai na ukatili wa utawala ghasibu wa Israel huko Gaza na kuamsha hisia za Waislamu dhidi ya Israel.
Abir Sa'di amesema, katika jumba hilo la elektroniki la Holocaust ya Gaza kuna picha na ripoti za jinai na mauaji ya Israel kwa lugha tofauti na pia silaha zinazotumiwa na Wazayuni dhidi ya raia wa Gaza.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi Habari ya Misri amesema kuwa, sehemu muhimu zaidi ya jumba hilo la makumbusho ni ile yenye picha za mauaji yaliyofanywa na Israel katika shule ya al Fakhoora inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi wa Palestina hapo tarehe 6 Januari. Wapalestina wasiopungua 43 waliuawa shahidi katika mashambulio hayo. 347590
captcha