Kiongozi wa Wakatoliki ametoa witi huo alipokutana na ujumbe wa maaskofu wa kanisa hilo wa Kiirani huko Vatican, ambapo amesisitiza kwamba Iran inapasa kutumia nguvu yake kubwa katika kujaribu kumaliza mgogoro huo na hatimaye kurejesha amani na utulivu katika Mashariki ya Kati.
Papa Benedict amesema kuwa Kanisa Katoliki linaunga mkono mtu au kundi lolote lile linalofanya juhudi za kuimarisha amani na utulivu ulimwenguni. Amesema, Iran ni daraja la kuziunganisha nchi za Mashariki ya Kati na za Asia na kwamba kwa yakini inaweza kuwa na nafasi muhimu katika kurejesha amani katika eneo hilo nyeti.
Kiongozi huyo wa Wakatoliki duniani amewataka Wakatoliki nchini Iran kushirikiana na serikali na kuwataka maaskofu wa Iran kuwashawishi wafuasi wao waendelee kubaki nchini kwao ili washirikiana na serikali katika kustawisha nchi yao na kuiletea maendeleo ya kuridhisha.
Wafuasi wa Kanisa Katoliki nchini Iran wanapata 25,000. 349687