IQNA

ISESCO yalaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel

15:50 - January 19, 2009
Habari ID: 1733113
Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO limetoa taarifa likilaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wasiokuwa na ulinzi wa Ukanda wa Gaza ambazo zinepelekea kuuawa mamia ya watu.
Taarifa hiyo ambayo imeelekezwa kwa jumuiya za kimataifa hususan UNESCO imelaani vikali mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni dhidi ya taasisi za kielimu na kiutamaduni, misikiti, hospitali na makazi ya raia wa Gaza.
Taarifa ya ISESCO pia imezitaka jumuiya za kimataifa kusimamisha uvamizi wa Israel haraka iwezekanavyo na kuwafikisha mahakamani watenda jinai hizo.
ISESCO imeyataja mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza kuwa ni hatua ya kigaidi na kihalifu na ikaongeza kuwa mashambulizi hayo yanalaaniwa vikali na dini na vigezo vyote vya kimaadili. ISESCO imesema: Kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya jinai hizo za kutisha kinatia aibu na kuongeza kuwa, badala ya kufanya juhudi za kuimarisha amani na usalama, jamii ya kimataifa imeuruhusu utawala ghasibu wa Israel kuendeleza jinai zake dhidi ya wananchi wa Gaza kwa kunyamazia kimya vitendo vya utawala huo.
Taarifa ya ISESCO imezitaka nchi za Kiislamu kushikamana na kuchukua haraka maamuzi madhubuti ya kuwasaidia wananchi wasiokuwa na ulinzi wa Gaza.
Mwishoni taarifa ya ISESCO imeyataka makundi mbalimbali ya Kipalestina kutupilia mbali hitilafu zao, kuungana mbele ya adui dhalimu, kukomboa ardhi zao na kujenga Palestina huru. 341571

captcha