Ujenzi na ukarabati wa misikiti ya zamani na mikongwe pamoja na maeneo ya historia ya Kiislamu na uimarishwaji wa utalii katika nchi za Kiislamu ni miongoni mwa mambo ambayo yamejadiliwa katika kikao hicho.
Qahtan al-Jaburi, Waziri wa Utalii wa Iraq, Hamid Ali Muhammad, balozi wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu, watafiti na wataalamu wa mambo ya kale pamoja na wahusika katika sekta ya utalii ya Iraq ni baadhi ya watu wanaoshiriki katika kikao hicho. Uporwaji mali na athari za kale za Iraq na Wamarekani katika kipindi cha vita vya uvamizi wa nchi hiyo nchini Iraq ni miongoni mwa mambo yaliyopewa kipaumbele katika ajenda ya kikao hicho.
Balizo wa OIC amesema katika kikao hicho kuwa jumuiya hiyo iko tayari kushirikian na viongozi wa Iraq katika kurejesha nchini humo athari na vitu hivyo vya historia ya kale ya Iraq. 350714