Warsha hiyo ambayo ni sehemu ya mpango wa mazungumzo ya kiutamaduni kati ya Ujerumani na Yemen, imetayarishwa na ubalozi wa Ujerumani mjini Sana'a, Chuo Kikuu cha Sana'a na Chuo Kikuu Huria cha Berlin.
Warsha hiyo inayowashirikisha wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu vya Yemen na Ujerumani inachunguza mtazamo wa Magharibi kuhusu ulimwengu wa Kiislamu na maisha ya Waislamu.
Malengo mengine ya warsha hiyo ni kuondoa mtazamo mbaya kuhusu dini ya Kiislamu, kuimarisha uhusiano kati ya Waarabu na nchi za Magharibi, kuchunguza matukio ya Ukanda wa Gaza na kushirikiana katika kuzuia matukio mengine kama hayo. 350647