IQNA

Maandamano dhidi ya Israel mjini Ankara

9:07 - January 20, 2009
Habari ID: 1733312
Zaidi ya watu elfu 30 wamefanya maandamano mjini Ankara Uturuki wakipinga jinai zilizofanywa na utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Waandamanaji hao ambao walikuzanyika kuitikia wito wa jumuiya na harakati za Kiislamu, walibeba bendera za Palestina na Uturuki na kutoa nara zinazoilaani Israel na mauaji yaliyofanywa na utawala huo dhidi ya wananchi wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Gaza.
Waandamanaji hao pia walikuwa na mabango yenye maandishi kama vile "Israel muuaji", "Heko kwa Hamas", Sisi sote ni wapiganaji wa Hamas", Palestina haiko peke yake" na Palestina imeshambuliwa kwa sababu wananchi wake ni Waislamu." 350573

captcha