Kwa mijibu wa gazeti la Peninsula, mabalozi hao wanatazamiwa kumkabidhi Rais Obama mapendekezo hayo ambayo wanataraji yatakuwa msingi wa sera za uhusiano wa baadaye wa nchi za Kiislamu na serikali ya Marekani.
Mapendekezo hayo yatakuwa ni pamoja na jinsi ya kuarifishwa Uislamu sahihi kwa nchi zisizo za Kiislamu na hasa Marekani, na kwamba ni dini inayohubiri amani na misimamo ya wastani katika jamii.
Lengo la mapandekezo hayo ni kukuza na kuimarisha uhusiano bora kati ya nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu.
Katika siku za mwanzoni za uongozi wake nchini Marekani, Barack Hussein Rais Obama anakusudia kutoa hotuba katika mojawapo ya nchi za Kiislamu na kubainisha sera za serikali yake katika kuamiliana na ulimwengu wa Kiislamu kuhusiana na masuala mbalimbali.
Lengo la hatua yake hiyo ni kupunguza changamoto ambazo zimejitokeza kati ya serikali ya Marekani na ulimwengu wa Kiislamu na hasa hasira ambayo imeongezeka katika nchi za Kiislamu dhidi ya serikali ya Marekani kutokana na siasa mbovu zilizotekelezwa na Rais Bush dhidi ya Uislamu na Waislamu katika kipindi cha utawala wake nchini humo.
Obama aliapishwa jana kuwa Rais mpya wa Marekani na wa kwanza mwenye asili ya Afrika katika historia ya nchi hiyo. 351421