Kwa mujibu wa tovuti ya Energy Publisher, hoteli hizo ambazo zinaendeshwa kwa misingi ya sharia na mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu, zinazidi kufanya vyema katika utoaji huduma na hivyo kuwavutia wateja wengi duniani licha ya kudorora uchumi wa dunia unaoathiri uchumi wa mashirika na nchi nyingi duniani.
Ripoti ya tovuti hiyo inasema kuwa, wakazi wa nchi tajiri za Mashariki ya Kati wana nafasi muhimu katika kuimarisha shughuli za hoteli hizo. Inasema, mwaka uliopita wa 2008, wakazi wa nchi hizo walitumia dola bilioni 12 katika safari zao za nje ya nchi.
Mbali na Waislamu wa eneo la Masharikiya Kati, wateja Waislamu wa nchi za Marekani, Ulaya, Afrika Kaskazini na maeneo mengine ya dunia walikuwa wateja wakubwa wa hoteli hizo katika kipindi hicho. Lengo la Waislamu kuvutiwa na hoteli hizo ni kuwa wanaweza kutumia chakula na kunufaika na vipindi vya burudani vinavyoandaliwa katika huduma zinazotolewa katika hoteli hizo kwa misingi ya mafundisho ya Kiislamu.
Wataalamu wa mambo wametangaza kuwa faida ya hoteli hizo hivi sasa ni zaidi ya dola bilioni 60, kiwango ambacho kinaonyesha ongezeko kubwa la faida.
Takwimu hizo pia zinaonyesha kuongezeka kwa hoteli hizo kwa kiwango cha asilimia 20 kwa mwaka. 351340