Kituo cha mafunzo ya Qur'ani na masuala ya kiutamaduni kinachofungamana na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu, ISESCO, kimefunguliwa mjini Kuala Lumpur, Malaysia.
Kwa mujibu wa gazeti la ar-Raya la Qatar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia, wawakilishi wa ISESCO, Wizara ya Elimu ya Malaysia pamoja na vyuo vikuu vya nchi hiyo wamehudhuria sherehe za ufunguzi wa kituo hicho.
Washiriki wa sherehe hizo walifanya vikao mbalimbali vya ushauri na kujadili masuala ya kiidara, mafunzo na uendeshaji wa kituo hicho muhimu cha Kiislamu.
Kituo hicho kimejengwa kwa ushirikiano wa ISESCO na serikali ya Malaysia.
Mbali na kufundisha masuala ya kidini, masuala yanayohusiana na shughuli za elimu na utamaduni za ISESCO ulimwenguni na hasa katika nchi za Kiislamu, yatakuwa yakijadiliwa na kuchunguzwa katika kituo hicho. 351841