Kikao cha kimataifa cha 'Quds, athari na historia' kitafanyika tarehe 30 mwezi huu wa Januari mjini Cairo, pambizoni mwa maonyesho ya 41 ya kimataifa ya vitabu.
Tovuti ya Muhit imesema kuwa, kikao hicho kimeandaliwa na Baraza la Kimataifa la Misaada na Uhubiri wa Kiislamu kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Waandishi ya Misri.
Waandaaji wa kikao hicho wanasema kuwa, waandishi na watafiti bingwa katika nyanja za historia ya Kiislamu ya Quds Tukufu watahudhuria kikao hicho na kuwasilisha makala mbalimbali kuhusiana na athari za kale za Quds.
Kujibiwa madai ya Wazayuni kuhusiana na athari za historia ya Quds na kuwasilishwa njia za kukabiliana na njama zao za kutaka kuifanya Quds kuwa ya Mayahudi ni miongoni mwa masuala yatakayopewa uzito katika kikao hicho.
Wataalamu na viongozi wa taasisi, jumuiya na mashirika mbalimbali ya Kiislamu watahudhuria na kuzungumza katika kikao hicho. 351921