IQNA

Kumalizika kikao cha kimataifa cha 'fatuwa na vipimo vyake' huko Makka

11:18 - January 22, 2009
Habari ID: 1734246
Kikao cha kimataifa cha 'fatuwa na vipimo vyake' kimemalizika hivi karibuni katika mji mtakatifu wa Makka kwa kutolewa taarifa.
Gazeti la Arabnews, limeripoti kuwa, katika taarifa hiyo maualama na wanazuoni walioshiriki katika kikao hicho wametaka kufikishwa mahakamani wahusika wote wa mauaji ya umati na jinai zilizotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia huko katika Ukanda wa Gaza. Wamevitaka pia vyuo vikuu vyote vya fiqhi na taasisi nyinginezo za Kiislamu kushirikiana katika kutatua matatizo yanayowakabili Waislamu ulimwenguni.
Taarifa hiyo pia imezitaka serikali za Kiislamu kuwaruhusu wanazuo kutekeleza majukumu yao vilivyo na kwa msingi wa mafundisho ya Kiislamu bila ya kuingiliwa kati masuala yao wala kutolewa mashinikizo ya kisiasa dhidi yao. Pia imewataka wanazuoni wa Kiislamu kuzuia utolewaji ovyo wa fatuwa na watu wasiofaa kufanya hivyo.
Vyombo vya habari pia vimeombwa kutangaza fatuwa zinazotolewa na watu waliohitimu masomo husika ya Kiislamu tu.
Taarifa hiyo iliyotolewa katika mji mtakatifu wa Makka pia imetaka kubuniwa kwa baraza kuu la utoaji fatuwa ili kuratibu shughuli za taasisi za fatuwa katika ulimwengu wa Kiislamu.
Kikao hicho cha siku tano kilifunguliwa mjini Makka Jumamosi ya tarehe 17 Januari na kumalizika jana tarehe 21. 351928
captcha