Gazeti la Misri la al-Akhbar limeandika kuwa wanafikra na wasomi wengi wa Kiislamu wamehudhuria kikao hicho na kuchambua masuala mbalimbali yanayohusiana na ulimwengu wa Kiislamu.
Vitabu vya ubunifu na marekebisho, ubunifu na changamoto zilizopo, matatizo ya udikteta na uhuru wa kifikra na ubunifu na mfungamano wa masuala ya zama hizi na zijazo ni miongoni mwa mambo yanayojadiliwa katika kikao hicho. Kuhuishwa utamaduni wa Kiislamu na kuuhusisha na tamaduni nyinginezo za ulimwengu pamoja na kusisitizwa kuwa ubunifu wa kifikra ni urithi mkubwa wa fiqhi ya Kiislamu, ni masuala mengine yatakayopewa kipaumbele katika kikao hicho.
Ahmad at-Tayyib, Mkuu wa Chuo Kikuu cha al-Azhar amesema katika ufunguzi wa kikao hicho kwamba, kupingwa fikra ya ubunifu wa kifiqhi katika Uislamu ni kutoa nara tupu tu katika misikiti na minasaba mbalimbali ya kidini bila ya kubadilishwa na kuwekwa nara hizo katika vitendo, kwa madhara ya umma wa Kiislamu.
Akijibu baadhi ya madai yanayotolewa na baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu kwamba, mlango wa ijtihadi ulifungwa katika karne ya tano Hijiria, at-Tayyib amesema kuwa fikra kama hizo potofu zinazuia kubadilishwa na kutekelezwa kivitendo fikra za utamaduni wa Kiislamu katika maisha ya kila siku ya Waislamu. 351897