Katika kikao cha waandishi wa habari cha Kamati Kuu ya Kuandaa Sherehe za Alfajirji Kumi za Mapinduzi ya Kiislamu zilizofanyika jana Jumatano, Sayyid Alam al Huda, Msaidizi wa Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuyakurubisha Madhehbu ya Kiislamu mbali na kutoa heko kwa ushindi wa watu wa Gaza na vile vile kumbukumbu ya ushindi wa Mpinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesema kuwa: “Tumeshuhudia kuhudhuria kwa wingi Masuni katika sherehe na tamasha za kitaifa za ushindi wa mapinduzi”.
Msaidizi wa Mkuu wa Jumuiya ya Kuyakurubisha Madhehebu ya Kiislamu ameashiria nafasi muhimu ya jamii ya Masuni nchini Iran katika kuandaa sherehe za Alfajiri Kumi na kuongeza kuwa: “Kamati ya Jumuiya ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu imeandaa sherehe maalumu kwa wanachama wake 27 katika miji na mikoa mbalimbali hasa ile ya mipakani ambayo ina idadi kubwa ya jamii za Masuni”.
Kuhusiana na nafasi ya idara za utamaduni za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nje ya nchi katika kuwafahamisha Waislamu duniani kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu, Sayyid Alam al Huda amesema kuwa: “Makundi ya kujitolea ya wahubiri katika nchi mbalimbali kama vile Pakistan, Syria na kwingineko yanaisaidia Jumuiya ya Kuyakurubisha Madehehbu ya Kiislamu katika kufikia malengo yake”.
Sayyid Alam al Huda ameashiria harakati mbalimbali za Ayatullah Muhammad Ali Taskhiri Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuyakurubisha Madhehebu ya Kiislamu katika medani ya kimataifa na akasema, Ayatullah Taskhiri amehudhuria zaidi ya makongamano 60 ya kimataifa kama mwakilishi wa Waislamu a Kishia. Kati ya makongamano hayo ni lile la Jumuiaya ya Fiqhi ya Kiislamu ya Saudi Arabia na Kikao cha Kifiqhi cha Banki za Kiislamu. Amesema, kuhudhuria makongamano hayo ni hatua muhimu katika kuyakurubisha pamoja madhehebu ya Kiislamu.
Sayyid Alam al Huda ameashiria athari za Mapinduzi ya Kiislamu katika kustawisha maisha ya Waislamu wa Kisuni nchini Iran na kusema kuwa: “Kuongezeka idadi ya Maulamaa wa Kisuni katika vyuo vya kidini ambao pia huandamana na misafara ya Masuni katika ibada ya Hija na vile vile kuongoza swala katika misikiti ni kati ya mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu katika kuboresha maisha ya Waislamu Masuni Iran”. 352118