Hayo yamesemwa na Muhammad Hassan Raiszadeh, Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon alipokutana na wanachuo wa nchi mbalimbali za Ulaya, America na Asia mjini Beirut.
Raiszadeh ameongeza kuwa jamii ya mwanadamu inapaswa kutumia mazungumzo kama njia ya kutatua hitilafu. Amesema, Hayati Imam Khomeini (MA) alitumai kuwa siku moja silaha zitabadilishwa kwa kalamu ili medani za vita na umwagaji damu zibadilike na kuwa medani za mazungumzo na majadiliano ya kielimu na kiutamaduni.
Afisa huyo wa utamaduni wa Iran mjini Beirut ameongeza kuwa: "Uhusiano wa kiutamaduni kati ya Iran na Lebanon ni wa kina na kihistoria unaorudi nyuma karne nne zilizopta. Amesema utamaduni wa Iran umeathiriwa na utamaduni wa maulamaa wa eneo la Jabal Amil kama vile Imam Musa Sadr na vile vile kinyume chake utamaduni na siasa za Lebanon umeathiriwa na maulamaa wa Kiirani kama Imam Khomeini. Amesema kuwa Lebanon iliathiriwa kwa kiwango kikubwa na mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kutokana na msimamo wa mapinduzi hayo wa kuwatetea wanyonge.
Kuhusiana na mzungumzo kati ya Iran na Marekani, Raiszadeh amesema kuwa: "Tatizo baina ya Iran na Marekani linatokana na tabia za kutumia mabavu na kiburi cha watawala wa Washington na maadamu hawabadili mwenendo wao, tatizo la uhusiano litaendelea kuwepo.
Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Lebanon amezungumzia uhusiano wa mfumo wa Waliul Faqih na Demokrasia na kusema: "Sisi tunaamini kuwa mfumo wa utawala wa watu au demokrasia umekamilika Iran kwa maana yake halisi. Leo hii viongozi wote muhimu wa mfumo wanachaguliwa kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja na wananchi. Aidha mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umejengeka kwa msingi wa kura za wananchi ambao waliidhinisha katiba ya mfumo huo katika kura ya maoni".
Alipoulizwa ni kwa nini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono harakati za mapambano za Hamas na Hizbullah, Raiszadeh amesema kuwa: "Hatua ya Iran ya kuunga mkono kisiasa, kitamaduni na kimataifa harakati za Hizbullah na Hamas imejengekeka katika mantiki ya kuwapa himaya wanaodhulumiwa na kupambana na dhulma na hilo linatokana na mafunzo ya kidini. Uungaji mkono huo hauna mipaka ya kijiografia, kidini au kundi maalumu la watu". 352758