Benki kubwa zaidi ya Kiislamu ulimwenguni itafunguliwa mwaka ujao nchini Bahrain katika msimu wa joto. Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News, Benki hiyo ambayo inasemekana kuwa itaambatana kikamilifu na sheria za Kiislamu, itaanzishwa kwa rasilimali ipatayo dola bilioni 11 huko Manama, mji mkuu wa Bahrain.
Hayo yametangazwa na Sheikh Swaleh Abdallah Kamil, Mkuu wa Baraza la Umma la Benki za Kiislamu nchini Bahrain na kuongeza kuwa, nchi wanachama wa Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC, zitakuwa wawekezaji wakuu wa benki hiyo.
Amesema, Benki ya Ustawi ya Kiislamu pia itawekeza katika benki hiyo na kwamba watu binafsi pia wanaweza kuwekekeza katika benki hiyo ya Kiislamu.
Huku akiashiria mgogoro wa kifedha unaoendelea ulimwenguni, Sheikh Swaleh amesema kuwa hii ni fursa bora ya kuwekeza sehemu mbalimbali kwa msingi wa sheria za Kiislamu.
Mipango ya kuanzisha benki hiyo ilianza kutekelezwa miaka mingi iliyopita. 353030