IQNA

Kitabu cha "Qur'ani, Kitabu Kisicho na Nakisi" Kimechapishwa India

11:11 - January 25, 2009
Habari ID: 1735484
Kitabu cha "Qur'ani, Kitabu Kisicho na Nakisi" kimechapishwa nchini India kwa lugha ya Telugu.
Mwandishi wa kitabu hicho Sayyid Shakil Ahmad Anwar amefanya juhudi za kutoa dalili na hoja za kielimu na kihistoria kuthibitisha kwamba Qur'ani ni neno la Mwenyezi Mungu na haiwezi kuwa imebuniwa na mwanadamu.
Katika kitabu hicho ambacho kimeandikwa katika sura ya maswali na majibu, mwandishi amefanya jitihada kubwa za kuondoa baadhi ya ufahamu usiokuwa sahihi kuhusu aya za Qurani Tukufu na kujibu maswali yanayoulizwa kuhusu kitabu hicho.
Kitabu cha "Qur'ani, Kitabu Kisichokuwa na Nakisi" kimechapishwa katika mji wa Haidarabad na kina kurasa 224.
Kitabu hicho kimechapishwa kwa lugha ya Telugu ambayo inatumiwa mno na watu wa jimbo la Andhra Pradesh nchini India. 353081
captcha