IQNA

Mkutano wa Kituo cha Kimataifa cha Kumuarifisha Mtume wa Uislamu

13:35 - January 26, 2009
Habari ID: 1736136
Kikao cha kwanza cha Kituo cha Kimataifa cha Kumuarifisha Mtume wa Uislamu (saw) kitafanyika Jumanne ya kesho mjini Riyadh, Saudi Arabia kwa shabaha ya kuarifisha sira na suna za Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa wasiokuwa Waislamu.
Kikao hicho ambacho kitaongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu Abdullah Abdulmuhsin al Turki kitajadili pia stratijia za kituo hicho na sifa makhsusi za Mtume Muhammad (saw).
Suala jingine litakalopewa kipaumbele katika mijadala ya kikao hicho ni stratijia ya kumtetea Mtume Muhammad (saw) katika nyanja mbalimbali za kieneo na kimataifa.
Kikoa cha viongozi wa nchi za Kiislamu kilichofanyika hivi karibuni mjini Dakar Senegal kilisisitiza juu ya udharura wa kuanzishwa kituo cha kimataifa cha kumtetea Mtume Muhammad (saw). Kituo hicho kitakuwa na wadhifa wa kumuarifisha Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu kwa wasiokuwa Waislamu, kusahihisha ufahamu usiokuwa sahihi kuhusu mtukufu huyo na kufafanua suna na mwenendo wake katika kutatua matatizo mbalimbali ya kibinadamu.
Makao makuu ya kituo hicho yako Riyadh, Saudi Arabia. Kituo hicho kina matawi katika nchi kadhaa za Kiislamu. 822323
captcha