IQNA

Kongamano la "Watetezi wa Palestina" limeanza mjini Cairo

14:05 - January 26, 2009
Habari ID: 1736173
Kongamano la Watetezi wa Palestina lilianza jana katika makao makuu ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mjini Cairo kwa shabaha ya kuchunguza hali ya Palestina na wananchi wa Ukanda wa Gaza.
Kongamano hilo linajadili masuala kama vile mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Gaza, kadhia ya wakimbizi wa Palestina, ustawi wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina na ukoloni.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Katika Masuala ya Palestina na Ardhi Zinazokaliwa kwa Mabavu Muhammad Sabiih amesema kuwa kongamano hilo la siku tano linachunguza mipango ya kutaka kujipanua zaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel hususan baada ya mashambulizi ya kinyama ya utawala huo katika Ukanda wa Gaza ambayo yamepelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa maelfu ya watu.
Sabiih amesema, Israel inaendelea kukiuka haki za taifa la Palestina, ujenzi wa vitongoji vya walowezi na kushambulia raia wa Palestina na kwamba utawala huo umedhamiria kuifanya Quds Tukufu kuwa ya Mayahudi, kutokomeza utambulisho wa Kiarabu na kuyavunjia heshima maeneo matakatifu ya Waislamu na Wakristo. 353805

captcha