IQNA

Daktari wa Norway: Israel imefanya majaribio ya silaha mpya katika Ukanda Gaza

11:05 - January 27, 2009
Habari ID: 1736452
Modes Gilbert daktari aliyejitolea kwenda kuwasaidia wakazi wa Ukanda wa Gaza wakati wa mashambulizi ya kinyama ya utawala haramu wa Isrel, ametoa wito wa kufikishwa mahakamani viongozi wa utawala huo kwa kutenda jinai za kivita na akasema: Katika vita vya siku 22 huko Gaza, Israel ililifanya eneo hilo mahala pa kujaribia silaha zake mpya.
Dakta Gilbert amesema, Israel imetumia silaha mpya na zilizopigwa marufu huko Gaza na kwamba mabomu yaliyotumiwa na utawala huo yalisababisha majeraha ambayo yanawatatiza madaktari kuyatibu.
Daktari huyo wa Norway ambaye alikuwa akihudumu katika hospitali ya al Shifaa kwa siku 11 wakati wa mshambulizi ya siku 22 ya Israel huko Gaza amesema kuwa, Israel imekiuka sheria na thamani zote za kibinadamu na maeneo yote ya Ukanda wa Gaza yalishambuliwa na jeshi la utawala huo.
Amesema kuwa ametayarisha uchunguzi wa kitiba kuhusu silaha zilizotumiwa na Israel katika vita vya Gaza na kwamba ataikabidhi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai za Vita na taasisi za kutetea haki za binadamu.
Dakta Modes Gilbert amesema: Miongoni mwa mabomu ya kizazi kipya yaliyotumiwa na Israel huko Gaza ni mabomu yenye urani iliyohafifishwa ambayo yanasababisha maradhi ya saratani. Amesema kuwa watu wanaolengwa kwa mabomu hayo hufariki dunia baada ya miezi kadhaa.
Daktari Gilbert amesema, kama viongozi wa Israel wanapinga kwamba walitumia silaha za mauaji ya umati na mabomu yaliyopigwa marufuku kimataifa katika mashambulizi yao huko Gaza wanapaswa kufungua vivuko vya kuingia Gaza ili wataalamu wa kimataifa wachunguze athari za mshambulizi ya Israel katika eneo hilo na kutoa ripoti kamili kuhusu mashambulizi hayo.
Tabibu huyo wa Norway amesema: Katika kipindi cha siku 11 ya kuhudumu kwenye hospitali ya al Shifaa aligundua kuwa asilimia 90 ya wahanga wa mashambulizi hayo walikuwa raia, watoto wadogo, wanawake na watu wazima na kwamba asilimia kubwa ya majeruhi zaidi ya elfu tano ni watoto wadogo.
Dakta Modes Gilbert amemalizia kwa kusema kuwa misikiti mingi iliharibiwa katika mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa na jeshi la utawala wa ghasibu wa Israel huko Gaza na kwamba swali linalopaswa kuulizwa hapa ni kuwa, ni nini kingetukia duniani iwapo Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ingeshambulia hekalu moja tu la Mayahudi? 354367
captcha