IQNA

Vyuo vikuu vya Gaza vyatakiwa kujengwa upya

15:17 - January 27, 2009
Habari ID: 1736571
Umoja wa Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu unaofungamana na Shirika la Elimu , Sayansi na Utamaduni la jumuiya ya OIC (ISESCO), umetoa taarifa ukitaka kuwepo jitihada za haraka za ujenzi mpya wa haraka wa taasisi za kielimu na kiutamaduni za Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa al Arab Online, taarifa hiyo imesema kuwa: “Katika hujuma yao ya siku 22 huko Gaza askari wa Israel waliharibu Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza pamoja na taasisi nyingi za kielimu, shule na maktaba katika eneo hilo la Palestina.
Taarifa hiyo imetoa wito kwa jamii za Kiarabu na Kiislamu, mashirika ya kieneo na kimataifa katika sekta ya elimu ya juu kufanya juhudi za kutosha za kutoa misaada ya kifedha, kiufundi na kielimu kwa taasisi za masomo na vyuo vikuu vya Gaza.
Umoja wa Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu pia umelaani vikali hujuma ya kinyama ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni iliyopelekea kuuawa shahidi watu wasio kuwa na hatia huko Gaza.
Jumuiya hiyo imetaka viongozi wa Kizayuni wafikishwe mbele ya mahakama ya kimatiafa ya jinai ya The Hague kutokana na jinai zao za kivita.
Umoja wa Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu pia umewataka wanachama wa umoja huo kukata uhusiano wowote ule na vyuo vikuu vya utawala wa Kizayuni.
Umoja wa Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu unajumuisha vyuo vikuu 330 vya nchi za Kiislamu. 354505
captcha