IQNA

Chuo kikuu cha kwanza cha Qur'ani magharibi mwa Afrika

11:50 - January 28, 2009
Habari ID: 1736921
Mipango ya awali ya kuzindua chuo kikuu cha kwanza cha Kiislamu katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria, imekamilika na chuo hicho kitafunguliwa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa tovuti ya Leadership Nigeria, chuo kikuu hicho ambacho kimejengwa pambizoni mwa msikiti wa An'yas katika mji wa Kano, kinafungamana na chuo kikuu cha Bairo na kitakuwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu ya Nigeria.
Chuo hicho kitakuwa cha kwanza cha elimu ya juu cha Qur'ani katika eneo la magharibi mwa Afrika.
Waislamu ambao ndio wengi kati ya wakazi wa kaskazini mwa Nigeria wanaunda asilimia 55 ya jamii nzima ya nchi hiyo. 354928
captcha