Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Saudi Arabia (SPA), kongamani hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Fiqhi ya Kiislamu na linahudhuriwa na wataalamu na wasomi wa masuala ya uchumi wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa Abdul Salam Dawud al Ebadi Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Fiqhi ya Kiislamu, kongamano hilo litachunguza sababu za kuzuka mgogoro wa sasa wa kiuchumi duniani na namna nadhari za kiuchumi za Kiislamu zinavyoweza kutumiwa kwa ajili ya kutatua mgogoro huo. Aidha watachunguza namna mfumo wa benki za Kiislamu unavyoweza kutumiwa ili kupungua matatizo ya kifedha katika nchi za Kiislamu na vile vile kuimarisha uwekezaji wa Kiislamu.
Kongamano hilo litahudhuriwa na wawakilishi wa Baraza Kuu la Shughuli za Benki na Taasisi za Kifedha za Kiislamu la Saudi Arabu, Kituo cha Utafiti wa Kiislamu cha Benki ya Maendeleo ya Kiislamu, Jumuiya ya Kimataifa ya Uchumi na Uwekezaji wa Kiislamu, Kituo cha Utafiti wa Uchumi wa Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Abdul Azizi cha Saudi Arabia na Kitengo cha Uchumi cha Chuo Kikuu cha Umul Quraa cha Makka.
Wataalamu kutoka taasisi hizo watawasilisha makala kuhusu nafasi ya uchumi wa Kiislamu katika kutatua mgogoro wa kiuchumi duniani. 355063