Kwa mujibu wa gazeti la Ar-Rayat, Bi. Dhafia Muhammad al Mari Mkurugenzi Mtendaji wa tamasha hiyo amesema kuwa: "Kutakuwepo na mashindano ya kuhifadhi, kusoma na kufasiri Qur'ani Tukufu pamoja na kusoma kwa pamoja aya za Qur'ani na kuwasilisha mada kuhusu ufahamu wa Qur'ani".
Bi al Mari amesema kuwa tamasha hiyo ya siku tatu itajumuisha wanawake walio na umri wa miaka 15-18 na kuongeza kuwa kutakuwa na programu nyinginezo za kidini, kiutamaduni mbali na mihadhara ya wanawake wasomi wa kidini wa Qatar.
Bi. Dhafia Muhammad al Mari amesema kuwa lengo la kufanyika tamasha hiyo ni kuimarisha utambulisho wa kidini wa wanawake vijana na kukuza utamaduni wa kuhifadhi na kusoma Qur'ani na kufahamu maana na mafunzo ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu. 355778