IQNA

Kufunguliwa ofisi ya IQNA kusini mashariki mwa Asia

10:24 - February 01, 2009
Habari ID: 1738242
Ofisi ya Shirika la Kimataifa la Habari za Qur’ani IQNA itakayokuwa ikisimamia masuala ya habari ya eneo la kusini mashariki mwa Asia imefunguliwa Alkhamisi iliyopita huko Bangkok mji mkuu Thailand, kwa mnasaba wa kuadhimishwa mwaka wa 30 wa Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na vilevile kuzaliwa kwa Imam Muhammad Baqir (as).
Ofisi hiyo imefunguliwa katika jengo la Taasisi ya Qur’ani ya Rasul al-A’dham (saw).
Mbali na kusimamia habari za shirika la Iqna zitakazokuwa zikitarjumiwa katika lugha ya Kitai ofisi hiyo itakuwa pia ikitarjumu na kutayarisha habari zitakazokuwa zikitumwa kwa lugha ya kifarsi katika makao makuu ya Iqna.
Watu wote waliohutubu katika sherehe za ufunguzi wa ofisi hiyo walielezea kufurahishwa kwao na hatua ya wakuu wa shirika la habari la Iqna ya kufungua ofisi ya shirika hilo huko Thailand kwa ajili ya kuhudumia shughuli na habari za Qur’ani katika eneo hilo la dunia. Wamesema, kwa kutilia maanani kwamba ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa unapitia kipindi kigumu cha hujuma ya kiutamaduni ya madola makubwa ya Magharibi kwa ajili ya kuharibu na kupotosha thamani za kidini na za Qur’ani Tukufu, kuna udharura mkubwa wa kutumiwa nguvu kazi yenye uzoefu na tajiriba kwa ajili ya kulinda thamani hizo.
Taasisi ya Qur’ani ya Rasul al-A’dham ina shughuli nyingi za kidini na Qur’ani nchini Thailand ikiwa ni pamoja na kuchapisha magazeti na vitabu vya kidini, kutoa mafunzo kwa walimu na kuandaa maonyesho mbalimbali ya kitaifa na vilevile shughuli za uhubiri wa dini. 356496
captcha